首页/Detail

斯瓦希里语奇幻

奇幻:魔法、异世界和想象力,让你想一口气读完的故事。按你的水平(入门至精通)阅读和聆听斯瓦希里语,附音频、翻译和测验。

关于奇幻的斯瓦希里语课程

奇幻高级
Taifa Leo8月31日

Huzuni Mfalme Oyo wa Tooro nchini Uganda akifariki; chanzo bado hakijatajwa

KAMPALA, Uganda: MFALME Oyo Nyimba Kabamba Iguru Rukidi IV wa Tooro Uganda alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 34. Waziri Mkuu wa ufalme huo, Calvin Armstrong Rwomiire Akiiki, alitangaza kifo chake Alhamisi usiku. Mfalme huyo alifariki mwendo wa saa nne usiku, bila kilichosababisha mauti yake kusemwa hadharani. Oyo alitwaa ufalme 1995 akiwa na umri wa miaka mitatu, baada ya kifo cha babake, Rukirabasaija Patrick David Matthew Kaboyo Olimi III, na kuwa mfalme mwenye umri mdogo zaidi duniani. Uganda ni jamhuri inayoongozwa na rais aliyechaguliwa, lakini ina falme kadhaa za jadi ambazo zinaendelea kuwa na ushawishi mkubwa wa kitamaduni na kijamii, licha ya uwepo wa utawala wa urais. Tooro iko magharibi mwa Uganda, karibu na mpaka wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Akiiki alisema mfalme huyo hakuwa ameoa, lakini aliacha mrithi na mwendelezo wa uzazi wake ambao umehakikishwa. Kifo chake kimezua huzuni kubwa Uganda. Kiongozi wa upinzani Bobi Wine alisema: “Habari za kusikitisha sana! Roho ya Mfalme ipumzike kwa amani ya milele.”

奇幻入门
Taifa Leo8月31日

Maraga atimiza vitisho, aanika ripoti ya polisi aliyompa Ruto

JAJI Mkuu Mstaafu David Maraga ameonya kuwa Idara ya Polisi inayopendelea kisiasa inaweza kuingiza Kenya katika machafuko baada ya uchaguzi huku akimtaka Rais William Ruto kutekeleza kikamilifu Katiba. Bw Maraga alisema hayo Jumatatu alipoweka wazi mapendekezo ya Jopokazi kuhusu Mageuzi ya Polisi aliloongoza mnamo 2023. “Polisi wanaoegemea mrengo mmoja kisiasa ndio walikuwa kiini cha ghasia za 2007/2008. Wakenya hawapaswi kusahau kwamba vifungu vya Katiba ya 2010 kuhusu taasisi huru viliandikwa kwa damu hiyo,” akasema Bw Maraga. Wiki iliyopita, Bw Maraga alimpa Rais Ruto makataa ya siku saba kuchapisha ripoti ya jopo kuhusu mageuzi ya polisi iliyowasilishwa kwake, akisema atachapisha mwenyewe iwapo serikali haitafanya hivyo. SOMA PIA: Maraga ampa Ruto siku saba achapishe ripoti iliyopendekeza mageuzi ya polisi lau sivyo aitoe yeye Alisema jopo lilipendekeza idara huru ya polisi ili kukomesha kile alichokiita kutekwa kwa Huduma ya Kitaifa ya Polisi (NPS) na kutumiwa vibaya kwa idara hiyo. Hayo ni miongoni mwa mapendekezo zaidi ya 200 yaliyotolewa na kikosi hicho kulingana naye. Bw Maraga ametaka mapendekezo hayo yote kutekelezwa, yakiwemo kuhakikisha uhuru wa NPS na kubadilisha sare za polisi. Hata hivyo, alisema mabadiliko ya sare hayakuwa jambo la dharura. NPS ilizindua sare mpya wiki iliyopita. Alisema Kenya sasa inashuhudia kile alichowahi kukiita “vurugu za kisiasa zilizopangwa, magenge na polisi wenye misimamo ya kisiasa”. Alitoa mfano huo kutokana na ghasia zilizoshuhudiwa Homa Bay, Keumbu na Ol Kalou, pamoja na visa vya vurugu katika makanisa ya Kisumu, Nairobi na Witima. Katika kisa cha Homa Bay, watu wawili, akiwemo polisi mmoja, waliuawa na wengine 46 kujeruhiwa katika mapigano yaliyovuruga mkutano wa Linda Mwananchi. “Jibu la tatizo hili ni kutii Katiba na Huduma ya Kitaifa ya Polisi lazima iwe huru. Ni hitaji la kuvunja mfumo wa polisi wa kikoloni na kukomesha kutekwa kwa mfumo wa usalama na serikali,” akasema Bw Maraga. Alisema ingawa Katiba iko wazi kuhusu uhuru wa polisi, Sheria ya Marekebisho ya Sheria za Usalama ya 2014 iliondoa kinga hizo na kusababisha NPS itekwe. Jopo la Bw Maraga lilipendekeza kufutwa kwa marekebisho hayo ya 2014 lakini anadai mapendekezo hayo yalipuuzwa. Alisema pia sheria kuhusu umri iligeuzwa na matokeo yake yakawa kwa faida ya wazi ya kisiasa.

奇幻中级
Rai A Tanzania8月29日

Zaidi ya Visa 5,700 Vilivyothibitishwa huku DR Congo Ikianzisha Chanjo ya Ebola katika Mikoa ya Mashariki

KINSHASA, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo / RankWire. AI / – Mamlaka ya afya ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imezindua juhudi za chanjo ya Ebola huko Kisangani, mji mkuu wa Mkoa wa Tshopo, kwa lengo la kudhibiti mlipuko mbaya zaidi nchini humo kuwahi kurekodiwa. Wafanyakazi wa afya walio mstari wa mbele, timu za kukabiliana [...] The post Zaidi ya Visa 5,700 Vilivyothibitishwa huku DR Congo Ikianzisha Chanjo ya Ebola katika Mikoa ya Mashariki appeared first on Rai A Tanzania.

按等级学斯瓦希里语奇幻

其他斯瓦希里语主题

关于通过奇幻学斯瓦希里语的常见问题

为什么要通过奇幻学斯瓦希里语?
你关心的内容更能抓住注意力,而且同样的单词会在不同课程中反复出现。这种重复正是让词汇记得牢的原因。
斯瓦希里语奇幻应该选哪个等级?
选你能理解十个词里的大约九个的那个等级。每个主题都有入门至精通的课程,你可以从简单的开始,逐步升级。
这些斯瓦希里语内容免费吗?
免费。学习本身免费,附音频、翻译和测验。Premium提供无限练习和导出等额外功能。