സ്വാഹിലി-ൽ ഭക്ഷണം
ഭക്ഷണം: പാചകം, റസ്റ്റോറന്റുകൾ, ചേരുവകൾ, ഭക്ഷണമേശയുടെ സംസ്കാരം. ആരംഭക്കാരൻ മുതൽ മാസ്റ്ററി വരെ നിലവാരത്തിൽ, ഓഡിയോ, പരിഭാഷ, ക്വിസുകൾ എന്നിവയോടെ സ്വാഹിലി-ൽ വായിക്കൂ, കേൾക്കൂ.
ഭക്ഷണം സംബന്ധിച്ച സ്വാഹിലി പാഠങ്ങൾ
വാർത്തകൾ
എല്ലാ 4-ഉം കാണുകMaziwa yaisha madukani bei ikipanda katika maeneo mengi nchini
WAKENYA wanakabiliwa na uhaba wa maziwa katika maeneo mbalimbali nchini huku uzalishaji ukipungua na bei kupanda. Takwimu rasmi ya Shirika la Takwimu la Kenya (KNBS) inaonyesha kuwa maziwa yaliyochukuliwa na kuuzwa katika nusu ya kwanza ya 2026 yalipungua kwa asilimia 0.6 hadi lita milioni 513.32 kutoka milioni 516.34 katika kipindi kama hicho mwaka uliopita. Uhaba huo unashuhudiwa Nairobi, Nyeri, Kirinyaga, Embu, Mombasa, Homa Bay, Kisii na maeneo ya Nyanza na Magharibi. Hata hivyo, Kisumu bado ina maziwa ya kutosha katika maduka makubwa, ingawa baadhi ya maduka madogo yaliripoti uhaba na bei ya juu. Jijini Nairobi, nembo ya baadhi ya kampuni maarufu kama Brookside, Mt Kenya, New KCC na Tuzo zimekosekana katika sehemu ya kuuza maziwa kwenye maduka ya Naivas Moi Avenue. Mtaani Donholm, mteja mmoja alisema bei ya pakiti ya maziwa ilipanda hadi Sh75 kutoka Sh60, huku wanunuzi wakiruhusiwa kununua pakiti tano pekee. Willy Kimani, mwanzilishi wa Duka la maziwa la Jaza, alisema wasambazaji wamemweleza kuwa mabadiliko ya hali ya hewa yamesababisha upungufu wa maziwa. “Kile ambacho wawasilishaji wa bidhaa wametuambia ni kwamba hali hii imetokana na mabadiliko ya hali ya hewa. Wameahidi kuwa hali itarejea kama kawaida mnamo Oktoba,” akasema Bw Kimani. Katika kaunti za Nyeri, Kirinyaga na Embu, nusu lita imepanda hadi Sh48 kutoka Sh44 kutokana na uhaba wa malisho ya mifugo. Wakulima wanaowasilisha maziwa kwa Kampuni ya Maziwa ya Mukurwe-ini, Nyeri wanasema uzalishaji umepungua kutoka lita 80,000 hadi 60,000. Mombasa na maeneo ya Pwani, pakiti ya mililita 500 imefikia Sh75 kutoka Sh60. Wafanyabiashara walisema mahitaji yameongezeka huku wasambazaji wakipunguza kiasi cha maziwa wanachopeleka madukani. Kule Homa Bay, bei ya katoni yenye pakiti 12 za mililita 500 imepanda kutoka Sh620 hadi Sh750. Kisii pia imeripotiwa kukumbwa na uhaba huo huku wauzaji wakipokea kiwango cha chini cha maziwa. - Ripoti za Kabui Mwangi, Gitonga Marete, George Munene, Winnie Atieno, George Odiwuor, Wycliffe Nyaberi na Domnic Ombok
Viongozi wa Kenya Kwanza wazidi kuunga mkono Mung’aro achaguliwe tutam
GAVANA wa Kilifi, Bw Gideon Mung’aro, amezidi kuungwa mkono na viongozi wa Kenya Kwanza kutetea kiti hicho katika Uchaguzi wa 2027. Spika wa Seneti, Bw Amason Kingi, alisema wanachama wa UDA Kilifi watamuunga mkono mgombea wa ODM. Hii ni licha ya kuwa, spika wa zamani wa Bunge la Kaunti ya Kilifi, Bw Jimmy Kahindi, alichapishwa kunuia kuwania ugavana kwa tikiti ya UDA miezi sita iliyopita. Akizungumza katika mkutano wa kisiasa Kilifi, Bw Kingi aliwataka wanachama wa UDA kutohisi wametelekezwa na uamuzi wa chama hicho kutowasilisha mgombea wa ugavana. Bw Kingi pia aliwataka wanachama wa UDA kutomuunga mkono mgombea wa ugavana ambaye atakuwa mpinzani wa Bw Mung’aro, akisema hatua hiyo itakuwa kinyume na makubaliano ya kisiasa kati ya vyama hivyo. Hata hivyo, Bw Mung’aro alisema yuko tayari kukabiliana na mgombea yeyote katika uchaguzi huo, akisema pia yuko tayari kushiriki mchujo wa ODM ili kupata tiketi ya chama hicho. Msimamo wa Bw Kingi unatofautiana na ule wa Katibu Mkuu wa UDA, Bw Hassan Omar, ambaye amekuwa akipinga mpango wowote wa kugawana maeneo ya kisiasa kati ya UDA na ODM.
ഭക്ഷണംഅഡ്വാൻസ്ഡ്Maono ya Rais Samia yazidi kupata msukumo, GEL yajenga kizazi cha sayansi na teknolojia
GEL yachochea mapinduzi ya elimu kuelekea Dira 2050 Na Mwandishi wetu KUNDI lingine la mamia ya wanafunzi wa Kitanzania wameondoka nchini Jumamosi kuelekea vyuo vikuu mbalimbali kuanza masomo ya elimu ya juu. Wanafunzi hao walioondoka jana kupitia Uwanja wa Ndege...
സംഭാഷണങ്ങൾ
എല്ലാ 120-ഉം കാണുകചെറിയ പ്രസംഗങ്ങൾ
എല്ലാ 120-ഉം കാണുകപോഡ്കാസ്റ്റുകൾ
എല്ലാ 4-ഉം കാണുകഭക്ഷണം
Wakati wa Chai Kila Asubuhi
Juma na Amina wanazungumza kuhusu desturi zao za chai kila siku, kutoka chai ya nyumbani hadi vibanda vya jirani, na kuangalia jinsi utamaduni wa chai unavyotofautiana duniani kote.
ഭക്ഷണം
Kupika Chakula au Kuagiza?
Juma na Amina wanazungumza juu ya tabia zao za chakula kila wiki. Wanalinganisha kupika nyumbani na kuagiza chakula. Wanashiriki mapishi rahisi, mila za kupika wikendi, na vidokezo vya kuokoa pesa na muda.
ഭക്ഷണം
Mapishi ya Bibi Yangu
Juma na Amina wanashiriki hadithi kuhusu vyakula vinavyopitishwa katika familia zao, kutoka mapishi ya mandazi ya bibi mwenye umri wa miaka themanini na nne hadi mchuzi wa nyama wa babu, na wanazungumzia jinsi ya kuendeleza mila hizi.
വീഡിയോകൾ
എല്ലാ 6-ഉം കാണുക
ആരംഭക്കാരൻ9:13INAUMA: Baba PATRICK Amwaga MACHOZI Alipoona JENEZA
Global TV Online
അപ്പർ-ഇന്റർമീഡിയറ്റ്15:30Sikiliza Hekima na Busara za Riziki Shahari na Zitto Kabwe Bungeni
Global TV Online
ഇന്റർമീഡിയറ്റ്20:15BABA MZAZI wa CARINA AJIBU NDUGU YAKE KUMROGA CARINA - SIRI NZITO - "SIKUTEGEMEA - SIYO KWELI"...
Global TV Online