홈/Detail

스와힐리어 음식

음식: 요리, 식당, 재료, 식탁 문화. 초급~마스터 수준에 맞춰 스와힐리어로 읽고 들어 보세요. 오디오, 번역, 퀴즈가 함께 있어요.

음식에 관한 스와힐리어 레슨

음식중상급
Taifa Leo8월 31일

Maziwa yaisha madukani bei ikipanda katika maeneo mengi nchini

WAKENYA wanakabiliwa na uhaba wa maziwa katika maeneo mbalimbali nchini huku uzalishaji ukipungua na bei kupanda. Takwimu rasmi ya Shirika la Takwimu la Kenya (KNBS) inaonyesha kuwa maziwa yaliyochukuliwa na kuuzwa katika nusu ya kwanza ya 2026 yalipungua kwa asilimia 0.6 hadi lita milioni 513.32 kutoka milioni 516.34 katika kipindi kama hicho mwaka uliopita. Uhaba huo unashuhudiwa Nairobi, Nyeri, Kirinyaga, Embu, Mombasa, Homa Bay, Kisii na maeneo ya Nyanza na Magharibi. Hata hivyo, Kisumu bado ina maziwa ya kutosha katika maduka makubwa, ingawa baadhi ya maduka madogo yaliripoti uhaba na bei ya juu. Jijini Nairobi, nembo ya baadhi ya kampuni maarufu kama Brookside, Mt Kenya, New KCC na Tuzo zimekosekana katika sehemu ya kuuza maziwa kwenye maduka ya Naivas Moi Avenue. Mtaani Donholm, mteja mmoja alisema bei ya pakiti ya maziwa ilipanda hadi Sh75 kutoka Sh60, huku wanunuzi wakiruhusiwa kununua pakiti tano pekee. Willy Kimani, mwanzilishi wa Duka la maziwa la Jaza, alisema wasambazaji wamemweleza kuwa mabadiliko ya hali ya hewa yamesababisha upungufu wa maziwa. “Kile ambacho wawasilishaji wa bidhaa wametuambia ni kwamba hali hii imetokana na mabadiliko ya hali ya hewa. Wameahidi kuwa hali itarejea kama kawaida mnamo Oktoba,” akasema Bw Kimani. Katika kaunti za Nyeri, Kirinyaga na Embu, nusu lita imepanda hadi Sh48 kutoka Sh44 kutokana na uhaba wa malisho ya mifugo. Wakulima wanaowasilisha maziwa kwa Kampuni ya Maziwa ya Mukurwe-ini, Nyeri wanasema uzalishaji umepungua kutoka lita 80,000 hadi 60,000. Mombasa na maeneo ya Pwani, pakiti ya mililita 500 imefikia Sh75 kutoka Sh60. Wafanyabiashara walisema mahitaji yameongezeka huku wasambazaji wakipunguza kiasi cha maziwa wanachopeleka madukani. Kule Homa Bay, bei ya katoni yenye pakiti 12 za mililita 500 imepanda kutoka Sh620 hadi Sh750. Kisii pia imeripotiwa kukumbwa na uhaba huo huku wauzaji wakipokea kiwango cha chini cha maziwa. - Ripoti za Kabui Mwangi, Gitonga Marete, George Munene, Winnie Atieno, George Odiwuor, Wycliffe Nyaberi na Domnic Ombok

음식마스터
Taifa Leo8월 31일

Viongozi wa Kenya Kwanza wazidi kuunga mkono Mung’aro achaguliwe tutam

GAVANA wa Kilifi, Bw Gideon Mung’aro, amezidi kuungwa mkono na viongozi wa Kenya Kwanza kutetea kiti hicho katika Uchaguzi wa 2027. Spika wa Seneti, Bw Amason Kingi, alisema wanachama wa UDA Kilifi watamuunga mkono mgombea wa ODM. Hii ni licha ya kuwa, spika wa zamani wa Bunge la Kaunti ya Kilifi, Bw Jimmy Kahindi, alichapishwa kunuia kuwania ugavana kwa tikiti ya UDA miezi sita iliyopita. Akizungumza katika mkutano wa kisiasa Kilifi, Bw Kingi aliwataka wanachama wa UDA kutohisi wametelekezwa na uamuzi wa chama hicho kutowasilisha mgombea wa ugavana. Bw Kingi pia aliwataka wanachama wa UDA kutomuunga mkono mgombea wa ugavana ambaye atakuwa mpinzani wa Bw Mung’aro, akisema hatua hiyo itakuwa kinyume na makubaliano ya kisiasa kati ya vyama hivyo. Hata hivyo, Bw Mung’aro alisema yuko tayari kukabiliana na mgombea yeyote katika uchaguzi huo, akisema pia yuko tayari kushiriki mchujo wa ODM ili kupata tiketi ya chama hicho. Msimamo wa Bw Kingi unatofautiana na ule wa Katibu Mkuu wa UDA, Bw Hassan Omar, ambaye amekuwa akipinga mpango wowote wa kugawana maeneo ya kisiasa kati ya UDA na ODM.

음식고급
JAMHURI MEDIA8월 30일

Maono ya Rais Samia yazidi kupata msukumo, GEL yajenga kizazi cha sayansi na teknolojia

GEL yachochea mapinduzi ya elimu kuelekea Dira 2050 Na Mwandishi wetu KUNDI lingine la mamia ya wanafunzi wa Kitanzania wameondoka nchini Jumamosi kuelekea vyuo vikuu mbalimbali kuanza masomo ya elimu ya juu. Wanafunzi hao walioondoka jana kupitia Uwanja wa Ndege...

레벨별 스와힐리어 음식

다른 스와힐리어 주제

음식으로 스와힐리어를 배우는 것에 대한 질문

왜 음식으로 스와힐리어를 배우나요?
관심 있는 콘텐츠는 집중력을 붙잡아 주고, 같은 단어가 여러 레슨에서 다시 나와요. 이런 반복이 어휘를 오래 기억하게 해 줘요.
스와힐리어 음식은 어떤 레벨을 골라야 하나요?
열 단어 중 아홉 단어쯤 이해되는 레벨을 고르세요. 모든 주제에 초급~마스터 레슨이 있어서 쉬운 것부터 시작해 올라갈 수 있어요.
이 스와힐리어 콘텐츠는 무료인가요?
네. 오디오, 번역, 퀴즈를 포함한 학습은 무료예요. Premium에서는 무제한 연습과 내보내기 같은 기능이 추가돼요.